Mashabiki 30,000 tu kushuhudia mchezo wa watani wa jadi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jul 2020
Mashabiki 30,000 tu kushuhudia mchezo wa watani wa jadi

Bodi ya Ligi imeweka hadharani viingilio vya mchezo wa nusu fainali kombe la FA kati ya Simba dhidi ya Yanga ambao utapigwa keshokutwa Jumapili kwenye uwanja wa Taifa

Viingilio hivyo vimefikiwa baada ya kikao cha pamoja cha shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), Serikali na vilabu vya Simba na Yanga

Majukwaa ya VIP A kiingilio itakuwa Shilingi 30,000/-, VIP B ni Shilingi 25,000/- wakati VIP C ni Shilingi 20,000/-.

Kwa majukwaa ya mzunguuko kiingilio kitakuwa Shilingi 10,000/-

Katika hatua nyingine Serikali imetangaza kuwa idadi ya mashabiki 30,000 pekee ndio watakaoruhusiwa kuingia uwanja wa Taifa kushuhudia mchezo huo

Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Singo amesema uamuzi huo umefikiwa kutokana na changamoto ya ugonjwa wa corona

Singo amesema tiketi zitakazouzwa kwa mashabiki ni 30,000 tu huku akiwataka mashabiki ambao watakosa tiketi wabaki nyumbani kushuhudia mchezo huo kupitia runinga

Amesema hawataruhusu watu ambao hawana tiketi kuzagaa eneo la uwanja wa Taifa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’