Kama unataka kwenda uwanja wa Taifa kushuhudia mchezo wa watani wa jadi hapo kesho, unapaswa kuhakikisha umepata tiketi yako leo kwani ni wazi mpaka kufikia kesho hakutakuwa na tiketi
Idadi kubwa ya mashabiki wameendelea kujitokeza kwa wingi katika vituo vinavyouza tiketi ikiwemo Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani Jijini Dar es salaam
Ni tiketi 30,000 ndizo zitakazouzwa , idadi ya mashabiki hao ndio wataruhusiwa kuingia uwanja wa Taifa kushuhudia mtanange huo wa kukata na shoka
ADVERTISE HERE