Kipigo hichi cha mabao 4-1 kinaingia kwenye historia ya vipigo vikubwa ambavyo Yanga imefungwa na Simba
Ni kipigo ambacho kwa hakika kilikuwa hakikwepeki kutokana na kiwango cha chini ambacho Yanga wameonyesha leo
Kipindi cha kwanza timu ilikuwa ikicheza chini sana, hakukuwa na nafasi yoyote iliyotengenezwa
Angalau kipindi cha pili timu ilijaribu kupandisha mashambulizi lakini kushambulia bila mpango kulipelekea Simba kutumia nafasi iliyokuwa ikiachwa na wachezaji wa Yanga waliokuwa wakipanda mbele kushambulia
Bao la kufutia machozi lilifungwa na Feisal Salum 'Fei Toto' kwa shuti la nje ya 18
Yanga imeondoshwa kwenye michuano ya kombe la FA kwa kipigo cha aibu
Matokeo haya yawe chachu ka uongozi pamoja na wadhamini GSM kuhakikisha wanafanyia kazi mapungufu yaliyopo Yanga ikiwa ni pamoja na kusajili wachezaji wenye ubora ambao watarejesha makali ya Yanga
Kwani kwa sasa tunaweza kusema Yanga imepoteza kabisa ubora wake, sio timu ya kuogopwa tena, heshima yake ya miaka mingi iko kwenye majaribu makubwa