Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Boniface Ambani raia wa Kenya amesema amesikitishwa na kipigo cha 4-1 ilichokutananacho klabu yake ya zamani kutoka kwa Simba.
Mkongwe huyo ameutaka uongozi kuboresha kikosi kwa sababu kimeonesha bado hakina uwezo wa kupigania mataji katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati
“Ni matokeo ambayo hayajanifurahisha hata kidogo, kufungwa nne na Simba haileti picha nzuri," amesema
"Viongozi wa Yanga waangalie na wajue kwamba hawana timu ambayo inaweza kupigania mataji katika ukanda huu"
"Mara ya kwanza nilipotazama mechi ya Yanga na Kariobangi Sharks haikunifurahisha na hapo niligundua timu ya Yanga haijakamilika. Usajili haukuwa mzuri lakini pia ule msukosuko wa Yanga umewafanya wasiwe na pesa ya kusajili wachezaji wazuri"
"Kipindi cha usajili kinakuja, hakuna haja ya kuwa na wachezaji zaidi ya 30 ambao hawaisaidii timu afadhali kuwe na wachezaji 25 wanaoweza kusaidia timu halafu pesa ambazo wanawalipa wachezaji hao zaidi ya watano watafute wachezaji wa maana wa kuisaidia klabu," aliongeza Ambani