Uongozi wa klabu ya Yanga umewataka, wapenzi, wanachama na mashabiki wake kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Singida United
Mchezo huo umepangwa kupigwa uwanja wa Taifa kuanzia saa moja usiku
Afisa Mhamasishaji Antonio Nugaz amesema ni muhimu kwa Wanayanga kuonyesha umoja wao kwa kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono wachezaji
Mchezo huo ni muhimu kwa Yanga kupata ushindi ili kuhakikisha inaweka hai matumaini ya kumaliza katika nafasi ya pili
ADVERTISE HERE