Eymael, Mabosi Yanga kujadili mkakati wa usajili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Jul 2020
Eymael, Mabosi Yanga kujadili mkakati wa usajili

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa watani zao Simba kimewapa taswira halisi ya aina ya usajili ambao wanapaswa kufanya kuelekea msimu ujao

Mbelgiji huyo amesema matokeo hayo yamewaumiza lakini anaamini yatawasaidia kusahihisha makosa katika usajili wa kukiimarisha kikosi chao kuelekea msimu ujao

"Nadhani kila aliyefuatilia ule mchezo aligundua mapungufu yetu yako wapi na sasa tunapaswa kuyarekebisha ili kuhakikisha msimu ujao tunakuwa na timu yenye ushindani"

"Tunapaswa kuwa makini kwenye usajili. Tunahitaji wachezaji bora watakaoweza kushindana na timu nyingine. Nimezungumza na viongozi kuhusu mkakati wa usajili na aina ya wachezaji ambao tunapaswa kuwa nao. Tutazungumza tena baada ya ligi kumalizika. Hatupaswi kurudia makosa " alisema Eymael

cut

Unaweza kusema usajili wa Yanga msimu huu unaomalizika ulikuwa wa 'kuunga-unga'. Idadi kubwa ya wachezaji waliosajiliwa na Mwinyi Zahera, kocha wa zamani wa mabingwa hao wa kihistoria waliachwa mwezi Januari, wakasajiliwa wachezaji wengine

Hata hivyo usajili huo bado umeshindwa kuifanya Yanga kuwa katika ubora na hivyo kushindwa kutimiza malengo waliyojiwekea

Eymael amesema wachezaji wote ambao watasajiliwa kuelekea msimu ujao lazima wakidhi vigezo ambavyo vitawekwa

Dirisha la usajili litafunguliwa wiki mbili zijazo, kuanzia August 01 na litafungwa August 31

Huenda kukashuhudiwa mabadiliko makubwa ya kikosi cha Yanga, wadhamini/wahisani GSM wakitenga zaidi ya Tsh Bil 1.5 kwa ajili ya zoezi la usajili

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’