Unamkumbuka yule 'Bwa Mdogo' ambaye baada ya mchezo dhidi ya Simba viedo yake ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii akilia kwa uchungu baada ya Yanga kufungwa maba 4-1?
Anaitwa Abdul Hassan, uongozi wa Yanga ulifanikiwa kumpata na kumualika kwenye mchezo dhidi ya Singida United uwanja wa Taifa leo akiwa miongoni mwa wageni mashuhuri 'VIP'
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Simon Patrick amesema wamejifunza mengi kupitia machozi ya mtoto huyo kufuatia matokeo dhidi ya Simba
Patrick ameahidi kuwa wataandika Historia baada ya msimu huu kumalizika
"Kupitia machozi ya mtoto huyu tumejifunza mengi, ujumbe umetufikia na tumejipanga kufanya mageuzi makubwa sana"
"Tuendelee kuitia moyo timu yetu, vijana wapambane wamalize msimu salama, baada ya hapo historia itaandikwa," amesema Patrick