Wachezaji hawakuwa sawa kisaikolojia - Eymael

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jul 2020
Wachezaji hawakuwa sawa kisaikolojia - Eymael

Licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Singida United, Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema vijana wake hawakuwa sawa 'kisaikolojia'

Mbelgiji huyo amesema wachezaji waliumizwa na kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Simba, hivyo walicheza mchezo huo kama wamelazimishwa

"Vijana wangu waliingia uwanjani wakiwa hawapo sawa kisaikolojia kwa maana walipoteza fahari yao, pesa na imani kwa mashabiki wao kutokana na matokeo ya mchezo uliopita wa jumapili dhidi ya Simba"

"Kufungwa ni kufungwa tu, hakuna sababu ya kupoteza matumaini. Haijalishi ukubwa wa kipigo kwa maana hata tungefungwa 5, 3, 2-1 ama tungefungwa kwa mikwaju ya penati bado uhalisia ungekuwa ule ule kuwa tumetolewa"

"Man City alifungwa goli 3-1 dhidi ya Liverpool lakini mwezi huu mwanzoni wakalipa kisasi kwa goli 4 - 0.Β  Huwezi kushinda mara zote ila inapotokea umepoteza unarudi kujipanga na kuhakikisha unashinda mchezo ujao, tutarudi imara zaidi msimu ujao," alisema Eymael

cut

Akizungumzia mchezo wa jana Eymael alisema kukosekana kwa umakini kwenye safu ya ushambuliaji bado ni changamoto kwani wangeweza kuibuka na ushindi mnono zaidi kama wangetumia nafasi nyingi walizotengeneza

"Tumeshinda dhidi ya Singida United japo tumepoteza nafasi nyingi za kutanua ushindi wetu, tatizo la kutotumia nafasi za kufunga tuzipatazo linajulikana na tutalifanyia kazi kama benchi la ufundi"

Yanga itashuka tena uwanja wa Taifa Jumamosi, Julai 18 kuikabili Mwadui Fc

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
4h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’