Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema anahitaji kusajili wachezaji wapya saba ambao wataingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza
Mbelgiji huyo amesema kama akiwapata wachezaji hao, msimu ujao ana uhakika wa kuwa kikosi imara ambacho kitaweza kushindania ubingwa wa ligi kuu
Aidha Eymael amesema wachezaji 10 au 11 wataachwa ili nafasi zao zichukuliwe na wachezaji wapya huku akipunguza ukubwa wa kikosi chake kutoka wachezaji 30 mpaka 25
"Kama usajili utafanyika kulingana na mapendekezo yangu, basi tuna uhakika msimu ujao tutakuwa na timu imara ambayo sio kwamba itaweza kuwania ubingwa wa ligi kuu, bali hata kuvipa changamoto vilabu vikubwa hapa Afrika," alisema Eymael
"Tunahitaji kuwa na kikosi kipana, kila nafasi kuwa na angalau wachezaji wawili wenye uwezo wa juu ili ikitokea mmoja ameumia, basi mwingine anaweza kucheza nafasi yake bila kuwepo mapungufu yoyote"
"Kwa sasa kila mmoja anafahamu tuna mapungufu, kikosi chetu sio kipana, tukiwakosa baadhi ya wachezaji tunakuwa na wakati mgumu"
"Tunahitaji kusajili wachezaji wapya sio chini ya saba ambao wataingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza lakini pengine tunaweza kuachana na wachezaji 10 au 11 ambao nafasi zao zitachukuliwa na wachezaji wapya"
cutYanga tayari imeshaanza michakato ya usajili ambapo inaelezwa mpaka sasa nyota wawili wa kigeni na mzawa mmoja tayari wamepewa mikataba
Aidh beki Abdallah Shaibu 'Ninja' anatajwa kurejea Yanga akipewa mkataba wa miaka miwili
Ninja anafanya mazoezi na kikosi cha Yanga kwa mapendekezo ya Eymael ambaye alihitaji kuwa nae mazoezini ili kujiridhisha na uwezo wake