Yanga yampa ruhusa Morrison aende popote

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Jul 2020
Yanga yampa ruhusa Morrison aende popote

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa umefunga mjadala kuhusu mchezaji raia wa Ghana Bernard Morrison anayedai kuwa huru kuanzia juzi Julai 15 baada ya kumaliza mkataba wake wa miezi sita ambao anadai kuutambua

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema hawana muda wa kujibizana na mchezaji huyo wakimtaka achukue uamuzi wake ambao anaona unafaa

"Sisi hatutaki maneno maneno mengi, kama anasema hana mkataba Yanga basi na aende akasaini mkataba na timu nyingine, yeye si ni mchezaji mkubwa? Waandishi wa habari muende mkamshauri badala ya kila siku kuzungumza tu kuwa hana mkataba mwambieni aende akasaini mkataba mpya huko anakohitajika"

"Lakini pia madai ya kuwa hajalipwa mshahara kwa miezi miwili mwambieni atoe taarifa ya benki ili nanyi mjiridhishe kama ni kweli hajalipwa?," alisema Bumbuli

Hivi karibuni uongozi wa Yanga uliwataka wanachama na mashabiki wake kutulia kwani wanafahamu ni hatua gani watamchukulia mchezaji huyo kutokana na matukio yake ya utovu wa nidhamu

Inaelezwa Yanga haina mpango wa kuvunja mkataba wake, licha ya jitihada za waziwazi zinazofanywa na Morrison kushinikiza jambo hilo ili aondoke akiwa mchezaji huru

Mkurugenzi wa uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said juzi aliweka wazi kuwa Yanga iko tayari kumuuza Morrison kama itajitokeza timu kumuhitaji lakini sio vinginevyo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’