Bumbuli ataja sababu ya kuitaka nafasi ya pili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Jul 2020
Bumbuli ataja sababu ya kuitaka nafasi ya pili

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wamepania kushinda michezo yote mitatu iliyobaki ili kuhakikisha wanamaliza katika nafasi ya pili wapate fursa ya kulipa kisasi kwa watani zao Simba

Kulingana na kanuni za ligi kuu, kama Simba itafanikiwa kutwaa kombe la FA na Yanga ikamaliza kwenye nafasi ya pili, timu hizo zitakutana kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii ambao utakaribisha msimu mpya

"Maandalizi ya kuelekea mchezo dhidi ya Mwadui Fc yamekamilika, tumejipanga kushinda mchezo huo na hata ile mingine miwili ili tujihakikishie kumaliza katika nafasi ya pili"

"Tunafahamu kulingana na kanuni za ligi, kama tutashinda nafasi ya pili na watani zetu Simba watatwaa kombe la FA, basi tutaweza kukutana nao kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii. Hii itakuwa nafasi kwetu kujiuliza walitufungaje mchezo uliopita," alisema Bumbuli

Yanga itashuka uwanja wa Taifa kesho Jumamosi kuumana na Mwadui Fc katika mchezo ambao watahitaji kuondoka na alama zote tatu ili kuendelea kujikita katika nafasi hiyo ya pili

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
18h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’