Mechi ya mwisho uwanja wa Taifa leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Jul 2020
Mechi ya mwisho uwanja wa Taifa leo

Kikosi cha Yanga jioni ya leo kitashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Mwadui Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom ambao utapigwa saa moja usiku

Mchezo huo ni wa mwisho kwa Yanga kucheza jijini Dar es salaam msimu huu

Wakiwa na mkakati wa kupigania nafasi ya pili, ushindi katika mchezo huo utaendelea kuweka hai matumaini hayo

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema vijana wake wako tayari, akiwa na matumaini watafanya kile alichowaelekeza

Eymael amesema ni wachezaji wawili tu Haruna Niyonzima na Mapinduzi Balama ambao watakosa mchezo huo kutokana na majeraha

Lakini pia winga Bernard Morrison nae ameondolewa kikosini, licha ya taarifa kuwa ameuomba radhi kwa uongozi wa Yanga

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa kuiunga mkono timu yao katika mchezo huo wa mwisho kuishuhudia timu yao jijini Dar es salaam msimu huu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’