Eymael apewe uhuru wa kuchagua watu wa kufanya nao kazi

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
19 Jul 2020
Eymael apewe uhuru wa kuchagua watu wa kufanya nao kazi

Wakati mwingine ni vizuri timu inapoteua kocha mkuu aachwe apendekeze watu wa kufanya nao kazi katika benchi lake la ufundi

Utaratibu huu utaongeza uwajibikaji hasa pale timu inapokuwa haifanyi vizuri

Enzi za kocha Mwinyi Zahera, mara kadhaa aliingia kwenye mgogoro na uongozi wa Yanga akipinga kuletewa kocha msaidizi

Alikataa kufanya kazi na kocha Charles Mkwasa kwa kigezo kuwa ni kocha anayemuheshimu sana lakini wana falsafa tofauti

Hata Yanga ilipomteua Meckie Mexime kuwa msaidizi wake Zahera alikataa akiridhika kufanya kazi na Noel Mwandila

Na waliondoka wote pale ajira yake ilipositishwa mwezi Novemba 2019

Tayari kuna minon'gono kuwa kocha Luc Eymael naye hafurahishwi kufanya kazi na baadhi ya watu katika benchi lake la ufundi akienda mbali zaidi kusema anaweza kuondoka yeye kama mapendekezo yake hayatafanyiwa kazi

Eymael alitua Yanga na kocha wa viungo Riedoh Berdien ambaye ndiye aliyepaswa kuwa kocha msaidizi na baadae akamleta daktari mtaalamu wa viungo

Jopo la watu wengine kama kocha msaidizi, kocha wa makipa, Meneja na Mtunza Vifaa aliwakuta hapo Yanga

Hata hivyo inaelezwa Eymael anataka kocha msaidizi ampendekeze yeye pamoja na kocha wa magolikipa nafasi ambazo zinashikiliwa na Charles Boniface Mkwasa na Peter Manyika

Imekuwa ni kawaida kote duniani kocha mkuu anakuwa na uhuru angalau wa kupendekeza kocha msaidizi, kocha wa makipa na wataalam wa viungo

Hii ni kwa kuwa nafasi hizi zinategemeana lazima ziwe na watu ambao wanafahamiana na wanaweza kufanya kazi pamoja

Kunapokuwa na mgogoro kati ya kocha mkuu na kocha msaidizi ni lazima utaathiri mwenendo wa timu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’