Mshambuliaji wa Dhofar FC ya Oman, Elias Maguri amesema yuko tayari kurejea nchini Tanzania kucheza ligi kuu ya Vodacom kama timu zinazomuhitaji zitafikia ofa yake.
Maguri alionyesha kiwango kizuri kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Benin dhidi ya Tanzania ambapo alifunga bao la Tanzania lililowezesha Stars kupata sare ya bao 1-1 ugenini.
Mshambuliaji huyo ambaye bado yuko nchini amesema mkataba wake na Dhofar FC unamalizika mwakani lakini timu itakayokubali kumlipa angalau Mil 80 itaweza kumsajili kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.
Amesema kwa kiwango hicho ataweza kuvunja mkataba wake.
Kabla ya kutimkia Oman, Maguri amewahi kuzitumikia timu za Simba, Ruvu Shooting na Stand United kwa nyakati tofauti.

ADVERTISE HERE