Winga wa Mtibwa Sugar Salum Kihimbwa huenda akawa miongoni mwa wachezaji wazawa watakaosajiliwa na Yanga kuelekea msimu ujao
Inaelezwa baada ya mchezo wa ligi kuu kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga uliopigwa juzi Jumatano kwenye uwanja wa Jamhuri, nyota huyo aliwekwa 'mtu kati' na moja wa mabosi wa Kamati ya usajili Yanga
Yanga inaendelea kukisuka upya kikosi chake kuelekea msimu ujao, nafasi ya winga imepewa kipaumbele kama ilivyokuwa ile ya ushambuliaji
Wakati Tusila Kisinda kutoka AS Vita akitajwa kusubiri muda tu aweze kutangazwa kutua Jangwani, Kihimbwa anaweza kuwa pacha wake
Yanga imeongeza umakini kwenye usajili wake, michakato ikifanyika kimyakimya, usajili unatajwa kuwa umekamilka kwa zaidi ya asilimia 90, kinachosubiriwa ni msimu kufika tamati hapo keshokutwa, mambo yawekwe hadharani