Baada ya takribani ya miezi 10 ya mikiki mikiki ya ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2019-20, ligi hiyo inafika tamati leo kwa timu zote 20 kushuka dimbani
Pamoja na mbio za ubingwa kuhitimishwa mapema kwa Simba kutetea taji lao, vita kubwa imebaki katika timu zinazoshuka daraja pamoja na ushindani wa nafasi ya pili baina ya Azam Fc na Yanga
Singida United ilijihakikishia kuteremka daraja mapema tu, lakini mshikemshike umebaki kwa timu nyingine saba ambazo tatu miongoni mwao zinaweza kuungana na walima alizeti hao kama hazipata ushindi kwenye mechi zao za leo
Timu hizo ni Ndanda, Alliance Fc, Mbao Fc, Mbeya City, Mtibwa Sugar, Mwadui Fc na Lipuli
Timu tatu kati yao zitaungana moja kwa moja na Singida United kushuka daraja wakati timu mbili zinakwenda kucheza play-off kuwania nafasi ya kubaki ligi kuu na timu nyingine za daraja la kwanza zitakazokuwa zikiwania kupanda daraja
Baada ya kuwepo matumaini kuwa Tanzania inaweza kuongezewa nafasi za ushiriki wa michuano ya CAF msimu ujao, nafasi ya mshindi wa pili imekuwa na umuhimu mkali kwa vilabu vya Yanga na Azam Fc
Kwani timu itakayomaliza kwenye nafasi hiyo inaweza kuungana na Simba kucheza ligi ya mabingwa wakati timu ya tatu huenda ikashiriki michuano ya kombe la Shirikisho
Yanga wako Iringa kuumana na Lipuli Fc ambayo iko hatarini kuteremka daraja, ni mchezo ambao utakuwa na ushindani mkali
Kutegemeana na matokeo ya mchezo kati ya Prisons dhidi ya Azam ambao utapigwa uwanja wa Sokoine, Yanga inahitaji kushinda mchezo dhidi ya Lipuli huku ikiomba Azam Fc wafungwe au watoke sare ya Tanzania Prisons
Mechi zote za leo
