Mabao 13 msimu mmoja sio haba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Jul 2020
Mabao 13 msimu mmoja sio haba

Mcongomani David Molinga ni mchezaji aliyekumbana na ukosoaji sana kwenye klabu ya Yanga licha ya kuwa ndiye kinara wa kuzimufania nyavu msimu huu

Molinga amemaliza ligi akiwa na mabao 11 huku akifunga mabao mawili kwenye michuano ya kombe la FA na hivyo kufikisha mabao 13

Ni wazi, mahitaji ya Yanga kutoka kwake yalikuwa zaidi ya huduma aliyoitoa, lakini nyota huyo anastahili kupongezwa kwani kufunga mabao 13 katika msimu wa kwanza sio jambo dogo..!

Kwenye ligi, amehusika katika michezo 28 kati yake akicheza dk 90 michezo 10. Pamoja na kufunganga mabao 11, Molinga ametoa pasi tano za magoli

Hatma yake iko mikononi mwa viongozi wa Yanga, lakini kwa hakika kama atabakishwa pengine msimu ujao anaweza kufanya vizuri zaidi

Hii ni kutokana na kuwa ameshapata uzoefu wa ligi na atakuwa akifahamu nini anapaswa kufanya

Mkongwe, beki wa zamani wa Yanga Bakari Malima 'Jembe Ulaya' amesema anaamini Molinga anastahili kuongezewa mkataba Yanga

Mkataba wake unamalizika wiki ijayo na zipo taarifa kuwa ataelekea kwa miamba wa soka nchini Morocco RS Berkane kama atakosa mkataba mpya Yanga

Β 

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
5h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’