Aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael ni kama alishafahamu kuwa zama zake zimemalizika ndio maana jana 'akaropoka' kauli zisizo za kiungwana
Mpango wa kumbadili ulianza mapema tu, tena kabla ya mtafaruko wake na Kocha Msaidizi Charles Mkwasa na Kocha wa Makipa Peter Manyika
Yanga inakamilisha mchakato wa kuliunda upya benchi lake la ufundi, kocha wa zamani wa timu hiyo Hans Van Pluijm akiongoza orodha ya majina yanayotajwa kurithi mikoba ya Mbelgiji huyo
Lakini pia, jina la kocha wa zamani wa Simba Patrick Aussems nalo linatajwatajwa kuwa anaweza kuibukia Jangwani
Nje ya Pluijm na Aussems, yupi anaweza kuwa mrithi sahihi wa Eymael?
ADVERTISE HERE