Viongozi wa Kamati ya Utendaji Yanga wakiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu Simon Patrick leo walifika uwanja wa Uhuru kutoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Benjamin William Mkapa aliyefariki dunia wiki iliyopita
Zoezi la kuaga mwili wa Mzee Mkapa linaendelea uwanja wa Uhuru, litafika tamati kesho Jumanne na atasafirishwa kuelekea Masasi kijijini Lupaso kwa ajili ya mazishi siku ya Jumatano
Enzi za uhai wake, pamoja na majukumu yake ya Kitaifa, Mzee Mkapa alikuwa mdau mkubwa wa klabu ya Yanga

ADVERTISE HERE