Klabu ya Azam Fc inatajwa kuwa katika hatua za mwishoni kukamilisha usajili wa kiungo wa Yanga Mohammed Issa 'Banka', imefahamika
Nyota huyo kutoka visiwani Zanzibar inaelezwa amefikia makubaliano ya kusaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia wauza Ice Cream hao
Banka hajaonekana katika kikosi cha Yanga kwa muda mrefu kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi na uongozi wa timu hiyo
Alirejeshwa kikosini wakati wa maandalizi ya mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Simba lakini hakuonekana tena baada ya mchezo huo ambao pia hakupata nafasi ya kuingia kwenye kikosi
Ni mmoja wa wachezaji ambao mashabiki walikuwa na matumaini makubwa kwake, lakini majeraha ya mara kwa mara yalimfanya asionekane mara nyingi
ADVERTISE HERE