Habari kubwa toka jana ni hatua iliyochukuliwa na uongozi wa Yanga kumpa siku 14 nahodha wao Papy Tshishimbi kuamua kusaini mkataba wa kuendelea kukipiga na mabingwa hao wa kihistoria au aondoke
Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Simon Patrick ambaye pia alisisitiza kuwa hawana tena muda wa kubembeleza wachezaji
Baada ya kusikia kauli hiyo, Tshishimbi akaibuka huku akimponda bosi wake huyo kuwa sio mtu wa mpira
Mcongoman huyo alikwenda mbali zaidi, leo ameahidi kufanya mahojiano na redio moja maarufu nchini
Kitendo cha Tshishimbi kuamua kutumia 'media' kuwajibu mabosi wake, ni dharau
Yeye kama nahodha hapaswi kuwa mwanzilishi wa migogoro ndani ya Yanga
Anachokifanya Tshishimbi hakimnufaishi yeye wala Yanga, zaidi ni kuwapa faida hao wenye vyombo vya habari ambao muda mwingi wanajadili masuala hasi ya Yanga tu
Hii sio mara ya kwanza Tshishimbi kuzungumza masuala yake na Yanga kwa waandishi wa habari.
Rejea mahojiano yake aliyofanya mwezi March, kauli zake zikiwachefua mashabiki kabla ya juhudi za kumuongezea mkataba hazijafanyika
Sitashangaa kusikia kama Yanga itachukua uamuzi wa kuachana nae leo baada ya mazungumzo yake kwani ni wazi Mcongomani huyo ana ajenda yake
Hakuna mchezaji mkubwa kuliko klabu. Kama hafahamu Yanga imewahi kutimua kikosi kizima mara mbili na ikaanza upya na bado ikafanikiwa
Msimu huu uliomalizika, uongozi wa Yanga umeyumbishwa sana na nidhamu za wachezaji wake
Hili ni jambo ambalo linapaswa kuzingatiwa katika usajili unaoendelea kufanyika kuelekea msimu ujao