Kamati ya Maadili Yanga yamjadili Morrison

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Jul 2020
Kamati ya Maadili Yanga yamjadili Morrison

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema winga Bernard Morrison raia wa Ghana amepelekwa Kamati ya Maadili ya klabu hiyo kutokana na mfululizo wa makosa ya utovu wa nidhamu

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Patrick Simon amesema suala la nyota huyo linajadiliwa na kamati ya Maadili wakati wakisubiri maamuzi ya kesi aliyofungua TFF kuhusu mkataba wake

"Kwanza nimeshachoka sana habari za Morrison lakini ni kwamba kuna kamati ya maadili ya Yanga inashughulikia suala lake muda si mrefu watalitolea maamuzi kwa sababu baada kuwa yametokea matendo ya kujirudia kila siku ilibidi tumpeleke kwenye kamati ya maadili ambayo ni huru ambayo mimi sipo kwenye hiyo kamati," alisema Patrick

"Kwa hiyo wanafanya taratibu zao wameshamwalika kumsikiliza, watatoa uamuzi wao, sisi tunawasubiri wao pamoja na TFF watuambie maamuzi yao juu ya kesi yake"

Aidha akizungumzia hoja ya baadhi ya mashabiki ambao wametaka mchezaji huyo azuiwe kutumia jezi za klabu ya Yanga katika mechi anazocheza mchangani, Simon amesema wao kama viongozi hawaoni kama kuna sababu ya kufanya hivyo

"Hata akivaa jezi ya klabu huko mtaani sisi hatuna tatizo kwa sababu kuna mashabiki wengi huko wanavaa mitaani kwa hiyo kwetu sio tatizo. Sisi tunatafuta suluhisho la kudumu ambalo litapatikana muda si mrefu"

Patrick amesisitiza kuwa klabu ya Yanga bado inawajibika kumhudumia mchezaji huyo na kuwa hata kodi ya nyumba wanaendelea kumlipia mpaka sasa

"Tulimwambia atafute nyumba sisi tutalipia kwa hiyo nikisema amehama makazi nitakuwa nadanganya kwa watanzania. Sisi tunamlipia kodi na mpaka sasa hivi tunafanya hivyo"

Jana Morrison alikamatwa na Polisi baada ya kupishana kauli na maafisa wa Jeshi la Polisi waliosimamisha gari lake baada ya kulitilia shaka

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
55m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’