Mapema leo zilisambaa katika mitandao ya kijamii picha za mlindalango wa Kagera Sugar Ramadhan Charamanda akiwa ameshika kinachoonekana kuwa mkataba wa klabu ya Yanga
Bado hakuna taarifa rasmi kutoka kwa uongozi wa Yanga kuthibitisha kama Charamanda amesajiliwa na mabingwa hao wa kihistoria
Kwani hakuonekani kuwa na changamoto katika eneo la golikipa, Metacha Mnata, Farouk Shikhalo na Ramadhani Kabwili wanaonekana kutosha
Lakini kuna jambo linaweza kutokea kama Yanga itaamua kusajili mlinda lango mzawa, nalo ni kuachana na Mkenya Shikhalo ili nafasi yake asajiliwe mchezaji mwingine wa kigeni asiye golikipa
Kumekuwa na maoni kuwa Yanga haina haja ya kuwa na mlinda lango wa kigeni kwani wapo walinda lango wa ndani ambao wanafanya vizuri
Je nini kinakwenda kutokea? tusubiri...!