Pamoja na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Ihefu Fc, Mbao Fc imeshindwa kujitetea kubaki ligi kuu baada ya kushushwa daraja kwa mabao ya ugenini
Mbao ilifungwa mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa mkoani Mbeya
Wanaungana na Singida United, Lipuli, Ndanda Fc na Alliance kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao
Wakati huohuo Mbeya City imetetea nafasi yake ya kubaki ligi kuu baada ya kuifunga Geita Gold bao 1-0 na hivyo kuondoka na ushindi wa jumla wa mabao 2-1
Ihefu Fc imeongeza idadi ya timu za Mbeya zitakazocheza ligi kuu msimu ujao wakiungana na Prisons na Mbeya City
ADVERTISE HERE