Uongozi wa klabu ya Yanga umempongeza nahodha wake msaidizi Juma Abdul ambaye msimu uliomalizika aliweza kucheza mechi 30 kati ya 38 na kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi kwenye kikosi cha Yanga
Abdul pia alitoa pasi sita za mabao akiwa kinara wa kupika mabao ya Yanga
"Ahsante sana nahodha wetu Msaidizi Juma Abdul, Wananchi tunathamini mchango wako," ulisomeka ujume uliotumwa na Yanga kwenye mtandao wa kijamii
Abdul ni miongoni mwa wachezaji watano wa Yanga waliojumuishwa katika orodha ya awali ya wachezaji 30 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa VPL msimu wa 2019-20
Wengine ni David Molinga, Feisa Salum, Mapinduzi Balama na Deus Kaseke
Hongera Juma Abdul Mnyamani...!
ADVERTISE HERE