Mnahesabu? watatu tayari

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Aug 2020
Mnahesabu? watatu tayari

Usajili wa nyota watatu uliofanywa na Yanga katika kipindi cha siku mbili, umekuwa sapraizi kwa baadhi ya wadau waliokuwa wakibeza ahadi zilizokuwa zikitolewa uongozi wa Yanga pamoja na mdhamini wao GSM

Katika misimu mitatu Yanga haikuwa na ubavu wa kichumi hivyo pamoja na kuhusishwa na wachezaji wengi, ilishindwa kukamilisha usajili wao

Lakini usajili wa beki kisiki Bakari Nondo Mwamnyeto, umetuma ujumbe kuwa Yanga imemaanisha kile walichosema

Kutua kwake Yanga kunamfanya Mwamnyeto kuwa mlinzi ghali zaidi kuwahi kusajiliwa kwenye ardhi ya Tanzania kwani usajili wake umeigharimu GSM takribani Milioni 230

Lakini pia Yanga ikafanikiwa kumsajili mmoja wa mabeki bora kabisa upande wa kushoto Yassin Mustafa ambaye walikuwa wakimfuatilia kimyakimya licha ya tetesi nyingi kumuhusisha na Azam Fc

Zawadi Mauya hakuwa maarufu sana lakini wale waliokuwa wakimfuatilia watakubali kuwa ni moja ya usajili bora sana uliofanywa na Yanga

Huyu ni mtu sahihi katika nafasi ya kiungo mkabaji, aina yake ya uchezaji unaweza kumfananisha na kiungo wa zamani wa Azam Fc Himid Mao Mkami, ni mtu wa kazi kwelikweli

Huu ni mwanzo tu kwani wanaotangazwa sasa ni wachezaji wa ndani, bado majembe ya Kimataifa hayajaanza kuwekwa hadharani bila kusahau kocha mkuu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’