Jamaniee tuwekane sawa, katika tetesi zinazokuwa zinazungumziwa wakati huu wa usajili, haimaanishi kila mchezaji anayehusishwa na Yanga basi ni lazima asajiliwe
Wako wengi tu huwa wanahusishwa na wengine hata kufanya mazungumzo na mabosi lakini mwisho wa siku uamuzi wa kuwasajili au la utatolewa na viongozi kwa kufuata mahitaji ya timu
Sio vyema kuwalaumu viongozi kuwa kwa nini hawakuwasajili wachezaji flani kwa kuwa tu kulikuwa na tetesi kuwa wanawafuatilia
Sio vibaya kumfuatilia mchezaji kama timu inamuhitaji, lakini pia hakuna tatizo kuachana nae kama timu itaamua kufanya hivyo kwa sababu wanazozijua
Kama Yanga ingesajili kila mchezaji ambaye anahusishwa nayo basi pengine mpaka sasa ingekuwa na wachezaji 200
Kwa hapa Tanzania, tetesi nyingi kuihusisha Yanga, basi hilo linatosha kudhihirisha kuwa Yanga ni klabu kubwa sana
Kule barani Ulaya utasikia tetesi nyingi zikizihusisha klabu kama Real Madrid, Fc Barcelona, PSG, Manchester United, Manchester City, Bayern Munich, Liverpool, Juventus na timu nyingine zenye hadhi ya 'ukubwa'
Jambo jingine hapa Bongo tumeshuhudia baadhi ya timu zikiwakimbilia wachezaji ambao wanatajwa kuwindwa na Yanga
Hii inaweza kuwa mbinu ambayo inatumiwa na waandishi wa habari kuwatafutia dili wachezaji flani flani
Kwani kwa wakati huu, ukitaka mchezaji awe na soko, we sema tu anawindwa na Yanga!
Kwa miaka ya karibuni baadhi ya wachezaji wanaosajiliwa na Simba au hata Azam ukifuatilia lazima utakuta tetesi za mwanzo ziliwahusisha na Yanga
Lakini pia utaratibu huu wa tetesi unaweza kutumika na timu kwa faida
Zinaweza kuibuliwa tetesi kuwa Yanga wanamtaka mchezaji fulani kumbe hawamaanishi huyo
Hapa kuna timu zitaingia mkenge kwa kusajili wachezaji wasio huku Yanga ikinasa vifaa vyake bila ya bugudha kabisa