Wiki inayoanza kesho Jumatatu huenda ikawa ngumu kwa baadhi ya nyota wa Yanga kwani mabingwa hao wa kihistoria watawapa mkono wa kwaheri baadhi ya wachezaji ambao hawakuingia kwenye mapendekezo kwa ajili ya kikosi cha msimu ujao
Inaelezwa baadhi ya majina yanaweza kuwastua mashabiki kwa kuwa wengine ni wachezaji wanaowapenda sana lakini uamuzi wa kuachana nao umezingatia vigezo vilivyowekwa
Kwani Wanafamilia wa Yanga wamekuwa na shauku ya kuiona taswira mpya ya timu yao baada ya kupitia changamoto mbalimbali katika kipindi cha misimu mitatu
Wachezaji ambao panga linaweza kuwapitia ni wale wenye nidhamu mbovu, vinara wa migomo pamoja na wachezaji walioshuka viwango
Yanga imeamua kuachana na wachezaji hao mapema ili kuwapa muda wa kusaka timu nyingine katika muda wa usajili ambao dirisha limefunguliwa jana likitarajiwa kufungwa August 31