Aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Marcio Maximo ni miongoni mwa makocha wanaotajwa kuomba nafasi ya kuinoa klabu ya Yanga
Maximo alipata mafanikio makubwa akiwa kocha wa Stars kati ya mwaka 2007 na 2010 na alijiunga na Yanga mara ya kwanza Juni 2014 akiletwa nchini na aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga wakati huo Yusufu Manji
Hata hivyo alishindwa kufikia malengo na kujikuta anaonyeshwa mlango kutokea baada ya miezi sita tu
Kocha huyo raia wa Brazil anaamini kutofanikiwa kwake mara ya kwanza ilikuwa bahati mbaya na akipata nafasi nyingine atafanya vizuri
Maximo ni miongoni mwa makocha zaidi ya sitini ambao wametuma CV zao Yanga
Zipo taarifa kuwa hata kocha wa sasa wa Stars Etienne Ndayiragije amejitosa kuomba apewe majukumu hayo ya kuinoa Yanga
Uongozi wa Yanga umeahidi kuwa watakamilisha mchakato na kumtangaza kocha mkuu mapema kabla ya timu kuingia kambini katikati ya mwezi huu