Jana Yanga iliwapa mkono wa kwaheri nyota 14, miongoni mwao wakiwemo nyota wa kigeni watano
Mshambuliaji David Molinga, Yikpe Gnamien na Erick Kabamba walikuwa miongoni mwao
Wengine ni aliyekuwa nahodha Papy Tshishimbi ambaye alitikisa kiberiti akitaka aongezewe 'mapesa'. Mwingine ni Patrick Sibomana
Kwa hakika wachezaji hawa hawana wa kumlaumu kwani walipewa nafasi ya kutosha kudhihirisha ubora wao
Labda kidogo Erick Kabamba ambaye hakuwa akitumiwa mara kwa mara lakini bado hoja inabaki palepale kuwa mchezaji wa kigeni hasajaliwi na timu ili akuze kiwango chake
Ni bahati mbaya wameitumikia Yanga kwa muda mfupi lakini pengine uamuzi huu wa kuondolewa mapema unaweza kuwasaidia huko waendako kwa kuimarisha viwango vyao
Sisi Wanajangwani tunawatakia kila la kheri, tunawashukuru kwa mchango wao katika msimu uliomalizika