Kuachwa kwa winga Mrisho Ngasa kumewaumiza mashabiki wengi wa Yanga kutokana na maoni yanayotolewa na wanayanga kila kona
Deus Kaseke nae jambo hilo limeonekana kumgusa sana, kwani yeye, Ngasa na Juma Abdul walikuwa kama mapacha
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Kaseke aliweka picha za matukio mbalimbali kati yake na Ngasa akionekana kuguswa sana baada ya Uncle kuachwa kwenye kikosi
Uongozi wa Yanga ulitahadharisha mapema kuwa watachukua maamuzi magumu ya kuwaacha baadhi ya wachezaji ambao wanafahamu wengine ni vipenzi vya mashabiki
Lakini lengo lao kubwa ni kuona wanaunda upya kikosi imara ambacho kitaweza kuwapa furaha Wanayanga kuanzia msimu ujao



ADVERTISE HERE