Klabu ya Yanga imewasilisha barua kwa klabu ya Azam Fc wakitaka kumsajili kiungo wa timu hiyo Salum Abubakar 'Sureboy'
Hata hivyo Azam wamesema hawako tayari kumuuza kiungo huyo kwa gharama yoyote
Sureboy amebakisha mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Azam Fc
Msemaji wa Azam Fc Thabit Zacharia 'Zakazakazi' amekiri kupokea barua ya Yanga kumtaka Sureboy
Hata hivyo amesema hawako tayari kumuuza mchezaji huyo kwani ni nembo ya Azam
Tangu kuanza kwa wiki hii tetesi zinazomuhusisha Sureboy na Yanga zimeshika kasi
GSM wameonyesha utayari kuvunja mkataba wake uliobaki na Azam Fc ili aweze kukipiga Jangwani
ADVERTISE HERE