Tuko tayari kumpokea?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Aug 2020
Tuko tayari kumpokea?

Moshi mweupe unakaribia kufuka pale Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani mabosi wa timu hiyo wakikaribia kuweka hadharani jina la mrithi wa Luc Eymael aliyekuwa kocha Mkuu wa Yanga ambaye alitimuliwa kutokana na makosa ya ubaguzi wa rangi

Kila Mwanayanga ametegea siku akisubiri ujio wa kocha huyo mpya atakayebeba matumaini yao kuelekea msimu ujao

Tayari TFF imeweka hadharani kuwa Septemba 06 msimu wa 2020/21 utaanza, jana Yanga ilitangaza kuwa timu itaanza mazoezi siku ya Jumatatu, August 10 2020

Majina ya makocha kama Hans van Pluijm, Patrick Aussems na hata Mwinyi Zahera yamekuwa yakizungumzwa sana

Lakini tangu juzi jina la kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Etienne Ndayiragije limechomoza zaidi taarifa za ndani zikibainisha kuwa huenda ndiye atakayepewa jukumu la kuiongoza Yanga

Nafasi ya kocha msaidizi bado jina la Meckie Mexime, kocha wa Kagera Sugar limeendelea kuchomoza

Bila shaka mwishoni mwa wiki hii kuelekea wiki ya Mwananchi, mambo yote ikiwemo kikosi kamili cha msimu ujao kitawekwa hadharani

Tusubiri..!

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
45m ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
12h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
16h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
20h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
21h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’