Uongozi wa klabu ya Azam Fc umemruhusu kiungo wake Salum Abubakar 'Sureboy' kutua klabu ya Yanga
Afisa Habari wa Azam Fc Thabit Zacharia amesema walikuwa na nia ya kuendelea na Sureboy kwani ni mchezaji wao muhimu lakini nyota huyo wa timu ya Taifa ameshinikiza kuwa anataka kujiunga na Yanga
Zakazakazi amesema wamewaita Yanga mezani ili waweze kukamilisha usajili wa nyota huyo
Ni suala la muda tu, Sureboy atatambulishwa kutua kwa mabingwa hao wa kihistoria
ADVERTISE HERE