Aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Senzo Mazingiza amesema amevutiwa na jinsi Yanga inavyofanya mabadiliko ya mfumo wa Uendeshaji na anaamini kuna sehemu anaweza kuchangia katika Mabadiliko hayo
Senzo alijiuzulu Simba mchana wa leo na jioni akatambulishwa kujiunga na Yanga mbele ya Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said ambaye mara kadhaa amesema kuwa GSM haijawahi kushindwa jambo
Senzo amefichua kuwa huko alikotoka mambo hayapo kama yanavyoelezwa
Ukosefu wa weledi, Maamuzi ya Bodi kutoheshimiwa pamoja na usajili wa Morrison yanatajwa kuwa mambo yaliyomfanya ajiondoe Simba na kupanda basi la Mabadiliko la Yanga
Kuhusu suala la Morrison Senzo ameeleza kuwa hakukubaliana na usajili wa nyota huyo hasa ikizingatiwa alifahamu kuwa ana mgogoro wa mkataba na Yanga ambao ulikuwa bado haujatolewa maamuzi na TFF
Lakini pia ameeleza kumfahamu vizuri Morrison tangu wakati yuko Afrika Kusini kuwa ni mchezaji aliyefanya usumbufu katika kila klabu aliyocheza
Senzo ana uzoefu mkubwa kwenye masuala ya uongozi wa soka Barani Afrika
Mwaka 2010 alikuwa Mjumbe wa Kamati iliyoandaa michuano ya kombe la Dunia ambayo ilifanyika Afrika kwa mara ya kwanza huko Afrika Kusini
Anasifika kwa ubobezi wa soka la Afrika ametua Yanga kuongeza ufanisi na weledi katika uongozi
Inaelezwa Mazingiza kesho Jumatatu ndiye atakayeenda kuiwakilisha Yanga kwenye shauri la Morrison!