Wakati wadau wakisubiri taarifa rasmi kutoka kwa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu, kuhusu sakata la winga Bernard Morrison, taarifa za ndani zimebainisha kuwa Yanga inaelekea kushinda kesi hiyo
Shauri hilo lilianza kusikilizwa toka saa tano asubuhi na pengine jioni hii TFF watamaliza na kuwaeleza Watanzania maamuzi yaliyofikiwa
Jambo kubwa ni kuwa taarifa za ndani zimebainisha kuwa imeonekana mikataba yote miwili ya Morrison na Yanga ni halali
Muhimu tusubiri taarifa rasmi ya Kamati ambayo itatolewa baada ya shauri hilo kufikia tamati
ADVERTISE HERE