Yanga yambana msemaji wa Azam Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Aug 2020
Yanga yambana msemaji wa Azam Fc

Uongozi wa klabu ya Yanga umemtaka Msemaji wa Azam Fc Thabit Zacharia 'Zakazakazi' athibitishe tuhuma alizotoa dhidi ya Yanga kuwa ndio walioandika barua iliyodaiwa kuandikwa na kiungo Salum Abubakar 'Sureboy' akiomba aruhusiwe kujiunga na Yanga

Mapema jana ilisambaa barua kwenye mitandao ya kijamii iliyodhaniwa kuandikwa na Sureboy akiuomba uongozi wa Azam Fc usikilize ofa ya Yanga, wamruhusu ajiunge na mabingwa hao wa kihistoria

Jioni Msemaji wa Azam Fc akaibuka na kuituhumu Yanga kuwa ndio iliyoandika barua hiyo na kuwa ilipelekwa ofisini kwao na mtu wa Yanga ambaye hata hivyo hakumtaja jina zaidi ya kusema mtu huyo ndiye aliyekuwa akipeleka ofa za Yanga kumtaka Sureboy

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amemtaka Zakazakazi athibitishe tuhumu zake pamoja na kumtaja mtu huyo aliyewapelekea barua

"Kumekuwa na tabia ya wasemaji wa timu nyingine kutembelea nyota ya Yanga ili wapate umaarufu mitandao, hii tabia tunataka ikome kuanzia Sasa tutadili nao bila kusita"

"Kama Msemaji wa Azam Fc atashindwa kumtaja huyo mtu wa Yanga aliye peleka barua basi ajiandae kujibu mashitaka," alisema Bumbuli

Aidha Bumbuli amesisitiza kuwa Yanga haikuandika barua hiyo na haina sababu ya kufanya hivyo

"Hata ukiangalia barua yenyewe haina nembo wala jina la mtu yoyote wa Yanga"

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’