Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imemtangaza mshambuliaji Bernard Morrison kuwa mchezjai huru baada ya kushinda shauri lake la mkataba dhidi ya Yanga
Kamati hiyo iliyosikiliza shauri lake kwa siku mbili, imeeleza kubaini mapungufu mengi kwenye mkataba wake mpya wa miaka miwili aliosaini na Yanga
Lakini pamoja na mchezaji huyo kutangazwa kuwa huru, ametakiwa kurudisha fedha zote (dola 25,000+) alizochukua Yanga na pia amepelekwa Kamati ya Maadili baada ya kusaini mkataba na Simba wakati shauri lake na Yanga likiwa halijamalizika
Shauri hili linapaswa kuwa funzo, wakati mwingine viongozi wanapaswa kuwa makini wanapoingia mikataba na wachezaji
Kwa maoni yangu, uamuzi uliochukuliwa hautakuwa na maumivu pande zote kwani hata kama Morrison angeidhinishwa kuwa mchezaji wa Yanga asingepata nafasi ya kucheza kutokana na matukio aliyofanya
Lakini fedha atakazorudisha (zaidi ya Mil 60) zinaweza kutumika kusajili mchezaji mwingine bora zaidi