Nsajigwa awaambia Simba wapambane na hali yao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Nov 2017
Nsajigwa awaambia Simba wapambane na hali yao
Kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema tangu mwanzo wa msimu Yanga ilijiwekea malengo na kinachofanyika sasa ni utekelezaji wa malengo hayo.

Nsajigwa ameyazungumza hayo punde baada ya Yanga kuondoka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mbeya City.

Katika mahojiano yake na Azam TV, Nsajigwa alisema kinachofanywa na Yanga sasa ni kutimiza malengo yeke na si kushindana na Simba kama wengi wanavyodhani.

"Sisi hatushindani na Simba, wao ndio wanatakiwa kushindana na sisi, tuna malengo yetu tangu tunaanza msimu huu kwamba mwisho wa msimu tuwe watu fulani kwa hiyo sisi ndio lengo letu hata kama tukipata goli moja tunamsukuru Mungu tumepata ushindi. Hata tungepata goli moja dhidi ya Mbeya City sisi kwetu pointi tatu ndio tunazihitaji, hatupo kwa ajili ya kushindana na Simba sisi tunahitaji kupata matokeo mazuri."

Yanga iko nafasi ya tatu ikiwa na alama 20, alama mbili nyuma ya vinara wa ligi kuu ya Vodacom, Simba.

Msimu uliopita Yanga ilitwaa ubingwa kwa tofauti ya mabao baina yake na Simba baada ya timu zote kujikusanyia alama 68.

Mpaka sasa Simba imefunga mabao mengi zaidi kuliko Yanga hata hivyo tofauti ya mabao imepungua kwa kiasi kikubwa (+5) baada ya ushindi mnono wa Yanga dhidi ya Mbeya City.

Jumamosi ijayo Yanga itashuka kwenye dimba la Chamazi kuivaa Prisons wakati Simba itashuka kwenye dimba hilo kuivaa kuivaa Lipuli Jumapili, Novemba 26.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’