Kikosi cha Yanga leo kinatarajiwa kuingia kambini kuendelea na maandalizi ya mikiki mikiki ya msimu mpya
Ligi Kuu ya Vodacom itaanza Septemba 06, ratiba ya ligi hiyo ikitarajiwa kuwekwa hadharani leo
Mazoezi rasmi ya mabingwa hao wa kihistoria yalianza tangu wiki iliyopita, wachezaji wakifanya mazoezi wakitokea majumbani kwao
Kocha Msaidizi Mtaalam wa viungo Riedoh Berdien ndiye aliyepewa jukumu la kusimamia mazoezi, wakati ujio wa kocha mkuu ukisubiriwa
Taarifa za ndani zimebainisha kuwa tayari Yanga imepata Kocha Mkuu na wakati wowote atatangazwa pamoja na benchi lake la ufundi na wataanza kazi mara moja
Lakini pia, nyota wa kigeni waliosajiliwa na mabingwa hao wa kihistoria wanatarajiwa kuanza kuwasili kujiunga na wenzao baada ya anga kufunguka
Jana Mkurugenzi wa uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said alitua DR Congo kukamilisha michakato iliyokuwa imekwama, pengine atarejea na baadhi ya nyota