Tutarajie mambo mazuri kutoka kwa Yassin Mustapha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Aug 2020
Tutarajie mambo mazuri kutoka kwa Yassin Mustapha

Awali Yanga ilihusishwa kumuwania beki wa kushoto wa Rayon Sports, Erick Rutanga

Kwa nyakati tofauti, Rutanga mwenyewe alithibitisha kupewa mkataba wa awali na mabingwa hao wa kihistoria

Hata hivyo ujio wa mlinzi mahiri Yassin Mustafa ni kama umebadili upepo, baada ya mabosi wa Yanga kuachana na Rutanga

Ni kutokana na kiwango kizuri anachoonyesha Yassin kwenye mazoezi ya Yanga

Ni wazi msimu ujao, atapishana kule upande wa kushoto na Adeyum Saleh, mmoja wa wachezaji walionusurika na panga kali lililopitishwa na Yanga kwa kuacha wachezaji 17

Kwa sasa hapa Tanzania ukizungumzia walinzi mahiri wa kushoto, huwezi kukosa kutaja jina la Yassin

Kiwango kizuri alichoonyesha akiwa na Polisi Tanzania, kimemuhakikisha mkataba mnono kutoka kwa Mabosi GSM

Yanga haikuanza kumfuatikia Yassin dirisha hili la usajili, tangu mwezi Januari alikuwa kwenye rada za mabingwa hao wa kihistoria

Kama mambo yangekwenda vizuri, pengine angesajiliwa kabla ya Adeyum

Huu utakuwa msimu wake wa kwanza Yanga, mashabiki wakiwa na matumaini makubwa kutoka kwake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
7h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
11h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
12h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
12h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’