Wiki ya Mwananchi imezinduliwa rasmi jana Jumamosi mkoani Dodoma na Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dk Mshondo Msolla katika tukio lililofanyika viwanja vya Mashujaa
Kilele cha Wiki ya Mwananchi ni Jumapili ijayo, August 30 pale uwanja wa Mkapa mkoani Dar es salaam ambapo mabingwa hao wa kihistoria watatambulisha kikosi chao
Kabla ya Jumapili, matukio kadhaa yanatarajiwa kufanyika;
Jambo kubwa la kwanza ni uzinduzi wa jezi kuelekea msimu wa 2020/21. Mashabiki wameonyesha shauku ya kuzisubiri jezi hizo, uzinduzi unatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa, siku mbili kabla ya tukio litakalosimamisha jiji la Dar es salaam
Lakini pia Yanga inakusudia kuzindua duka lake rasmi la kuuza jezi na vifaa vingine vya michezo pale Makao Makuu ya klabu
Ujenzi wa Duka hilo tayari ulishaanza na pengine baada ya jezi kuzinduliwa zinaweza kuanza kuuzwa katika duka hilo
Aidha katika kipindi cha maadhimisho ya Wiki ya Mwananchi, Wanayanga watashiriki kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kwenye maeneo yao lakini kutakuwa na siku moja ambayo litaendeshwa zoezi la uchangiaji damu
August 30 ndio shughuli itaenda kuhitimishwa pale kwa Mkapa..!