Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wanatarajiwa mchezo wao wa kilele cha wiki ya Mwananchi dhidi ya Aigle Noir utapigwa saa moja usiku kutokana na muingiliano wa ratiba
August 30 mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba dhidi ya Namungo FcΒ utapigwa mapema saa tisa na nusu Alasiri
Bumbuli amesema kuepusha sontofahamu ya muingiliano wa ratiba, wataendelea shamrashamra nyingine wakati mchezo huo ukiendelea

Aidha kuhusu maandalizi kuelekea mchezo wa Jumapili, Bumbuli amesema kikosi kinaendelea vizuri na mazoezi, kiungo Carlos Fernandes 'Carlinhos' akiungana na wenzake leo
ADVERTISE HERE