Wakati wanachama na mashabiki wa Yanga wakisubiri kwa hamu ujio wa Kocha Mkuu Cerdric Kaze, inaelezwa Mrundi huyo huenda akachelewa zaidi baada ya kupata matatizo ya kifamilia
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapewa wiki hii, Kaze alitarajiwa kuwasili siku ya Ijumaa, lakini uwezekano wa kocha huyo kufika siku ni mdogo na pengine mabosi wa Yanga wanaweza wakalazimika kufanya maamuzi mengine kutokana na muda mchache uliobaki kabla ya ligi kuanza
Imeelezwa leo viongozi wanakutana kujadili suala hilo na hatma yake inaweza itategemea na maamuzi ya kikao hicho
Ikumbukwe Kaze aliwashinda wenzake wawili waliokuwa wamevuka mchujo wa makocha 64
Hivyo ni wazi kama kutakuwa na ulazima wa kumleta kocha mwingine huenda akatoka miongoni mwa wale wengine wawili
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mjumbe wa kamati ya mashindano Eng Hersi Said, Yanga inatarajia kuja na tangazo la hatima ya kocha baada ya kikao hicho