Kesho Ijumaa wadhamini wa klabu ya Yanga kampuni ya GSM, watazindua rasmi jezi za klabu hiyo kwa ajili ya msimu wa 2020/21
Jezi hizo zinazotajwa kuwa kwenye ubora zaidi ya msimu uliopita, zitaanza kupatikana madukani kesho hiyohiyo
Hii itakuwa nafasi kwa mashabiki kujipatia jezi mpya tayari kwa Tamasha la wiki ya Mwananchi siku ya Jumapili, August 30
Jumamosi Yanga itazindua duka lake pale Makao Makuu ya klabu, mashabiki wataweza kujipatia bidhaa zote za Yanga pale Makao Makuu
Duka liko katika hatua za mwisho kukamilika tayari kwa uzinduzi huo
ADVERTISE HERE