Bado Yanga haijatangaza jina la Kocha Mkuu baada ya kuachana na Cedric Kaze ambaye ameshindwa kuja kutokana na matatizo ya kifamilia
Kwa sasa mabingwa hao wa kihistoria wako chini ya Kocha Msaidizi Juma Mwambusi aliyeanza majukumu yake tangu juzi
Jina la kocha wa zamani wa TP Mazembe Hubert Velud limeibuka viungani tangu jana akitajwa kuwa huenda akaibuka kurithi mikoba ya Luc Eymael
Velud ni kocha mwenye 'CV' kubwa sasa akiinoa timu ya Taifa ya Sudan
Miongoni mwa timu alizowahi kuzinoa barani Afrika ni pamoja na Difaa El Jadida za Morocco, ES Setif, CS Constantine, JS Kabylie na USM Alger za Algeria, Etoile Du Sahel ya Tunisia na TP Mazembe ya DR Congo
Velud aliwapa TP Mazembe ubingwa wa Afrika mwaka 2016 lakini pia akishinda mataji ya Super Cup, ligi kuu ya DRC na kombe la Ligi
Kule nchini Algeria Velud alitwaa mataji mawili ya Ligi Kuu ya Algeria akiwa na ES Setif na USM Alger
Tayari Yanga imemtangaza kocha anayechukua nafasi ya Luc Eymael ni Zlatko Krmpotic raia wa Serbia