Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema ahadi walizotoa kwa Wanayanga kuelekea msimu mpya wamezikamilisha kwa asilimia 95
Aidha katika majojiano na Wasafi Radio mapema leo, Injinia Hersi alibainisha mambo kadhaa ambayo wameyafanya na wanayokusudia kuyafanya msimu huu;
βMwaka huu ni mwaka wa mabadiliko kwa klabu yetu ya Yanga, na tutafanya makubwa sana kimafanikio kama tulivyoahidi sisi GSM.
βGumu zaidi ilikuwa usajili wa Mwamnyeto ambaye wenzetu walishamtaja kama mchezaji wao lakini kuonesha tupo serious tulifanikisha kumchukua.
βLengo letu ilikuwa kujenga kikosi chetu, kiwe imara na kutupata matokeo. .kama wadhamini tumefanikiwa kwa asilimia kubwa sana.
βKama mdhamini hatuwezi kuwa katika klabu ambayo haiwezinkutupa matokeo, mwaka jana tulifanya kwa mapenzi yetu, lakin sasa tunafanya kwa dhana ya uwajibikaji.
βNimekuwa nafanya majukumu mengi ambayo sio taaluma yangu ndio maana tumemuajiri Senzo Mbatha mtaalamu wa haya mambo ili sisi tukae pembeni kama wadhamini.
βTumefanya analysis ya kutosha kabla ya usajili, tumefanya usajili kucover udhaifu wa kikosi chetu, Makipa tunao wazuri sana Metacha na Shirkalo wapo national team hapa ina maana tuna makipa bora sana lakini walikosa mafunzo sahihi ndio maana tumemleta kocha wa makipa bora kutoka Burundi.
βBeki ya kulia, kuna Kibwana Shomari, na kushoto yupo Yussuf katikati Mwamnyeto, baada ya kumpoteza Tshishimbi tumemleta mchezaji wa timu ya Taifa Congo huyu ni Top Player Tonombe Mukoko, kulia kuna mchezaji matata sana Tuisila Kisinda kushoto yupo Farid Mussa na wengineo matata sana.
β Kelvin Yondani na Juma Abdul hawana nafasi tena, maana tulishafunga usajili wa wachezaji wa ndani pia hakuna ukweli wowote kuhusu kumsajili Jack Tuisenge!
βTuna vikosi viwili, cha ndani ambacho hakimhitaji mgeni hata mmoja. . Metacha, Shomari, Yussuf, Ninja, Mwamnyeto, Zawadi Mauya, Kaseke, Feitoto, Waziri, Balama, Nchimbi.
βKuna aina 3 za umiliki, tupo katika hatua za kuchambua kila aina ya umiliki na faida zake ili kucomply na agizo la serikali kuwa 51% wanachama na 49 % mwekezaji.
βSenzo atakuwa mshauri wa utendaji wa klabu yetu, anakuja kufanya ushauri katika operation team. . atasimamia mikataba ya wachezaji na wafanyakazi, pia budget ya kuendesha klabu kisasa zaidi. .
βSenzo atasimamia mishahara, vyanzo vya mapato kusimamia na kuongeza na pia na mambo mengine ya kiutawala.
βTumeshare organogram na Senzo tumempa nafasi yeye apendekeze leadership structure ya klabu yetu.
βBaada ya siku ya wananchi Senzo atakuwa busy sana kuandaa set up nzima ya klabu yetu huku tukisubiri maelekezo kutoka La Liga.
βSenzo ana mkataba wa mwaka mmoja and there is a room for extension.
βJezi tutazindua rasmi na tutatoa utaratibu kupitia klabu yetu, jezi hii ina uzuri kuzidi mipaka. Jezi inakuja na concept yenye feature na uhalisia wa klabu yetu. .kuna changamoto ya kontena kuchelewa lakini mzigo utafika mapema na kutosheleza nchi zima.
βTuna jezi tatu, ya nyumbani ,ugenini na third kit. .
βKisinda na Mukoko ni wachezaji wakubwa , Mukoko anamilikiwa na As Vita , Tuisila anamilikiwa na Union Manyema alikuwa Vita kwa Mkopo. . usajili huu ndio ulinipa changamoto kubwa sana! tulivunja mikataba yao pia tuliwapa signing fees!
βCongo passport za wachezaji humilikiwa na vilabu, baada ya kuzipata tulipofika airport wachezaji walitakiwa kuwa authorised na klabu hivyo tukasubiri dk 45.
β Kuna watu walienda Ethiopia kumpokea Carlinhos, lakini hawakujua utaratibu wa Ethiopia. . ndugu zetu wa Simba SC walipoenda Ethiopia waliwekwa karantini kwa maana Ethiopia ipo karantini! walimpigia simu aliwaambia pesa haiwezi kumnunua yeye anaenda Yanga SC.
βMost expensive city in Africa ni Luanda Angola, Carlinhos ni mchezaji mwenye uwezo kifedha na amekuja Yanga SC kwa mapenzi yake mwenyewe,watu wamejaribu kuichafua klabu yetu ili asije lakini alishikilia msimamo Angola pia wameshangaa kwa kipaji chake atakujaje Tanzania?