Wakati akihojiwa mapema leo, Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said aliwataka Wanachana na Mashabiki wa Yanga wakae tayari kupokea jezi mpya zenye ubora wa hali ya juu
Wengi wameulizia jezi hizo zitawekwa hadharani muda gani hasa ikikumbukwa mwanzoni mwa wiki ilitangazwa kuwa zingezinduliwa leo
Injinia Hersi alisema Meli iliyobeba shehena ya jezi imechelewa kufika hivyo kuwataka mashabiki wawe na subira
Aidha Injinia alisema kuwa wanaleta mzigo wa kutosha nchi nzima hivyo mashabiki wasihofu kwani kila mmoja atajipatia jezi yake
Uzinduzi wa jezi mpya za Yanga unasubiriwa kwa shauku kubwa. Jezi hizo ambazo bado hazijawekwa hadharani zimemwagiwa sifa kemkem na wadau waliopata nafasi ya kuziona
Pengine hili ndilo jambo linalowafanya mashabiki wawe na shauku kubwa ya kuziona
Lakini pia kilele cha wiki ya Mwananchi ni keshokutwa Jumapili, mashabiki wanatamani kutinga pale uwanja wa Mkapa wakiwa ndani ya uzi mpya wa mabingwa hao wa kihistoria
Bila shaka GSM na Uongozi wa Yanga wanafanyia kazi maoni yanayotolewa na wadau juu ya umuhimu wa jezi hizo kupatikana mapema