Fei Toto ndio mtamjua sasa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Aug 2020
Fei Toto ndio mtamjua sasa

Kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' jana aliwapa furaha mashabiki wa Yanga baada ya kuionyesha kiwango kikubwa kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir maalum kuhitimisha wiki ya Mwananchi

Akicheza kiungo pacha na Mkongomani Mukoko Tonombe, Feisal alikuwa huru kuchezesha timu, pasi yake mpenyezo ilitendewa haki na Tuisila Kisinda aliyeifungia Yanga bao la kwanza

Huyu ndio Fei Toto aliyejiunga na Yanga akitokea visiwani Zanzibar misimu miwili iliyopita

Kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania Emmanuel Amunike, aliwahi kueleza kushangazwa kwa nini kiungo huyo mpaka sasa bado yuko nchini

Alisema Fei Toto anaweza kucheza hata kwenye kikosi cha timu kama FC Barcelona

Hakika maneno ya Amunike yana ukweli ndani yake, kama ataendeleza moto huu alioanza nao, Fei Toto hatamaliza msimu akiwa ndani ya kikosi cha Yanga

Huyu atailetea Yanga 'mapesa' ya kigeni. Habari njema Yanga wameliona hilo ndio maana wakampa mkataba wa miaka minne

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’