Krmpotic ameanza kazi leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Aug 2020
Krmpotic ameanza kazi leo

Kikosi cha Yanga jana kilishusha shoo ya kibabe kwenye mchezo dhidi ya Aigle Noir wakicheza mechi hiyo wakiwa na takribani siku tano tu chini ya kocha Msaidizi Juma Mwambusi

Kwa wiki mbili, Yanga ilikuwa chini ya kocha wa viungo Riedoh Berdien ambapo mwanzoni mwa wiki iliyopita ndipo kocha Juma Mwambusi akaungana nae baada ya Cedric Kaze aliyekuwa akisubiriwa kuchelewa na baadae kupata udhuru ambao uliifanya Yanga imtangaze Zlatko Krmpotic kuchukua nafasi yake

Nyota wengi wa kigeni walifanya mazoezi chini ya siku saba, hivyo kwa kiasi kikubwa, ile shoo ya jana ilitokana na uwezo binafsi wa mchezaji mmoja mmoja

Kuanzia leo Krmpotic ndio anaanza kukisuka rasmi kikosi chake akisaidiana na Mwambusi ambaye kwa kiasi kikubwa aliweza kuiandaa timu iliyocheza vizuri sana mechi ya jana

Huyu Krmpotic ni muumini wa soka la kushambulia, kwa kikosi alichonacho hakika ashindwe mwenyewe kwani Yanga ya sasa imekamilika kila idara

Leo mabingwa hao wa kihistoria huenda wakamshuhudia mshambuliaji Yacouba Songne akitua kwenye ardhi ya Tanzania kuzidi kuiongezea Yanga makali

Songne aliondoka Burkina Faso jana na anatarajiwa kuwasili nchini siku ya leo

Krmpotic ana siku tano za kukiandaa kikosi chake kabla ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons siku ya Jumamosi, saa moja usiku

Huu utakuwa mchezo wa kwanza wa kufungua msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom

Pengine ndani ya wiki nne, Krmpotic atakuwa tayari ametengeneza kikosi imara kitakachokuwa na kazi moja tu, kugawa dozi kwa kila anayekuja mbele!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’